
Mwenyekiti wa ICDT ndugu JUMA MAKONGORO akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bunda kuwakabidhi fedha milioni kumi ikiwa ni mchango wa wana ICDT kuwezesha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Sanzate.Machango huo katika sekta ya elimu unalenga ili kupunguza umbali wa kwenda shule kwa watoto wa eneo ambao husafiri umbali mrefu kwenda shule za jirani. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Bunda ndugu Changwa Mkwazu ametoa shukrani lwa ICDT kwa mchango.
Mkurugezi Mtendaji alikabidhi fedha hizo kwa bodi ya shule ili ujenzi huu uanze mara moja, kwa niamba ya Bodi ya Shule ua Sanzate Mwenyekiti ndugu Mkaka Katani alipokea fedha hizo.